KUHUSU SISI

Get Up Tanzania (GUTz) inatoa msingi kwa mashirika ya nchini na watu binafsi kufanya kazi pamoja katika kutangaza pia kutoa ujumbe kuhusiana na virusi vya ukimwi (VVU) na kuwezesha vijana wa kitanzania kufanya hivyo hivyo.

Muunganiko wa karibu baina ya washirika wa Dutch, Begian na Tanzania ndio unaoifanya GUTz kuwa ya kipekee. Nguvu yetu kubwa inatoka katika washirika na utayari tulio nao kwa pamoja: kuhamasisha vijana wa kitanzania kuchukua hatua ya muhimu sana katika vita dhidi ya virusi vya ukimwi (VVU). Kwa wakati huo huo mgawanyiko mzuri wa majukumu ni muhimu sana kwa uwazi baina ya washirika na wahisani na ustahimilivu na ukuaji wa  shughuli. Kwa taarifa Zaidi kuhusiana na majukumu ya asasi na shirika, tafadhali tazama kurasa husika.

Vision

Medical cross Icon HIV

Dhumuni kubwa la GUTz ni kuhamasisha vijana wa kitanzania kupima virusi vya ukimwi (VVU) na kutokusita kuongelea suala la virusi. Katika kila tamasha tunafanya kazi na wataalam wa afya na madaktari kutoka katika eneo husika. Zaidi ya hili, utafiti wetu huwa tunafanya kwa ukaribu zaidi na wahusika tofauti tofauti wa sekta ya afya kutoka serikalini wanaohusika na suala la VVU. Yote haya ni kuweza kufanya ufuatiliaji mzuri, utoaji wa ushauri nasaha na kuhakikisha matibabu yanapatikana kwa wale wote wanaokuwa wamebainika kuwa na virusi vya ukimwi (VVU) katika matamasha yetu.

Music note Icon

Kwa wakati mmoja wanamuziki na wanamaigizo hutoa ujumbe kwa wasikilizaji kuhusiana na suala zima la virusi vya ukimwi (VVU). Kwa kuweka wasanii wakubwa wa tasnia ya muziki na vikundi vya maigizo katika jopo letu na kutangaza uwepo wao katika matangazo yetu kwa jamii siku kadhaa kabla ya matamasha, tunavutia wasikilizaji na watazamaji kujitokeza kwa wingi katika eneo la tamasha; tunatengeneza mazingira huru ambayo inawezekana kuongelea kuhusu virusi vya ukimwi (VVU) na kuondoa dhana potofu ya uoga katika suala zima la kupima.

Education book Icon HIV

Kwa wakati mmoja wasanii wa muziki na maigizo hutaarifu wasikilizaji kuhusiana na suala la virusi vya ukimwi (VVU) na umuhimu wa kupima. Muingiliano wa maigizo unahusisha wageni ktk majadiliano kuhusu njia za maambukizo, jinsi ya kuzuia maambukizo na pia upimaji. Maelezo na elimu hayatoki kwa washirika wa GUTz pekee bali yanaundwa kwa pamoja na wasikilizaji na watazamaji wetu. Get Up Tanzania, tunasimama pamoja!

Heart Icon HIV

Tunaamini ya kwamba Tanzania ina wananchi wengi sana pamoja na mashirika ambayo yanatumia utayari wao na nguvu katika kufanya kazi kupunguza matatizo kama virusi vya ukimwi (VVU) katika jamii zao kwa namna tofauti tofauti. Kwa ubunifu ikijumulishwa na hizi juhudi kutoka katika Nyanja mbalimbali ndani ya jamii ya kitanzania itatengeneza mabadiliko makubwa sana. Pamoja twaweza “Get Up” kukabiliana na haya matatizo na kuweza kufanya mabadiliko ya hali ya juu.

Optimization WordPress Plugins & Solutions by W3 EDGE