26.000

Jumla ya waliohudhuria

8.638

Watu waliopima

531

VVU+

Kuangalia video wetu.

Utambulisho wa GUTz

Makadirio ya watu wapatao 1.4 milioni nchini Tanzania wanaishi na virusi vya ukimwi (HIV). Kuongelea kuhusu virusi na usambazwaji wake bado ni nadra sana na vijana wengi wa kitanzania bado hawajui hali zao za kiafya na umuhimu wa kupima katika mazingira ya kawaida ya kiafya. Muunganiko wa hatari:Watu wasiojua hali zao za kiafya ndio wasambazaji wakubwa wa virusi kwa wengine na hivyo kufa kutokana na magonjwa yanayoendana na UKIMWI.

Get Up Tanzania (GUTz) inahamasisha vijana wa kitanzania kuchukua hatua ya muhimu katika upambanaji dhidi ya virusi vya ukimwi (HIV): Kwa kujitokeza na kupima!

Kwa wengi wao, kwenda katika zahanati zinazotambulika ni hatua kubwa na ya kuogopesha kwa wao kuichukua. Katika matamasha yetu maarufu ya elimu kupitia burudani tunatoa huduma za elimu ihusianayo na virusi vya ukimwi (HIV) na pia tunafanya upimaji katika njia ambayo ni ya kipekee nay a mvuto. Wasanii wakubwa wa muziki hutoa burudani na pia vikundi vya maigizo hufanya maonesho mazuri kuhusiana na virusi vya ukimwi (HIV), yote hii ni kwa ajili ya kuhamasisha wageni waliohudhuria katika tamasha kuweza kupima hapo hapo. Utaratibu huu wa GUTz unafanya kazi vizuri kuliko kawaida, watu hupanga foleni katika sehemu zetu za kufanyia upimaji hadi mda wa kufunga umapowadia.

Tangia tamasha letu la kwanza mwaka 2013, tumeshakaribisha Zaidi ya wageni 26,000 katika matamasha madogo na makubwa na zaidi ya watu 9000 wamepima virusi vya ukimwi (HIV). Watu 531 kati ya wote walioshawahi kupima kupitia matamasha yetu tayari wanajua wana virusi vya ukimwi (HIV) na muhimu Zaidi tayari tumewaunganisha na vituo vya afya kwa ajili ya kupata ushauri nasaha na matibabu ya bure kupitia serikali.

GUTz Foundation (NL+BE)

GUTz Foundation inatafuta fedha zinazohitajika kwa ajili ya uwezeshaji wa shughuli za GUTz Organization na pia kutoa mafunzo kwa washirika wa Tanzania juu ya utafutaji wa watu wa kujumuika nao na wafadhili wa nchini, utafiti, uundaji wa mipango kazi & taarifa na utengenezaji wa muundo imara wa shirika. Kipindi tunaweka ukaribu baina ya shirika na asasi tunaangalia Zaidi ubora wetu: Uwazi na Uimara. GUTz Foundation imeanzishwa nchini Netherlands mwaka 2014 na baadae nchini Belgium mwaka 2016.

GUTZ organization (TZ)

GUTz Organization ndipo haswa mambo yakipekee yanapofanyika: Shirika la kitanzania huungana na mashirika ya tiba nay a kiserikali kuwezesha ufanyikaji wa matamasha mahali ambapo yanahitajika Zaidi. Tangia mwaka 2016, NGO ya kitanzania imekuwa na wajibu wa uandaaji wa shughuli zote na utafutaji wa misaada na ufadhili wa hapa hapa nchini. Tunashukuru kwa kazi nzuri ya washirika wetu kutoka Tanzania, tumeonda ukuaji mkubwa sana katika idadi ya watu wanaojitokeza kupima afya zao na pia msaada wa karibu kabisa kutoka katika mashirika na serikali ya Tanzania.

Michango ya hiari

Kwa kiasi cha Tsh. 9600 utakuwa umempa au umewapa watu nafasi ya kuchukua hatua ya kwanza kuhusiana na virusi vya ukimwi (HIV): kupata elimu na kufanya upimaji. Tafadhali fikiria kutoa mchango wako wa hiari!
Kama utapendelea kutoa mchango wa hiari kupitia katika akaunti yako ya kibenki moja kwa moja, tafadhali tumia maelekezo yafuatayo hapo chini. Kama unahitaji maelezo ya ziada kuwa huru kuwasiliana nasi kupitia barua pepe info@gutz-foundation.org

PROJECTS

image

Suzanne

Founder & Director

Stichting Gutz (NL)

image

Nyakwesi

Managing director

NGO GUTz (TZ)

image

Gideon

Financial Director

NGO GUTz (TZ)

image

Reuben

Medical advisor

NGO GUTz (TZ)

image

Jimmy

Theatre Coach

NGO GUTz (TZ)

image

Kathy

Board Member

VZW GUTz (BE)

image

Elise

Board member

Stichting GUTz (NL)

image

Wouter

Board member

Stichting GUTz (NL)

image

Danny

Board Member

VZW GUTz (BE)

Optimization WordPress Plugins & Solutions by W3 EDGE